Idadi ya watu waliofariki kwenye tetemeko la ardhi lililotokea nchini
Italia Jumatano hii imeongezeka na kufikia watu 247.
Tetemeko hilo linalokadiriwa kuwa na nguvu ya 6.2 katika
vipimo vya Ritcher limesababisha madhara makubwa kwenye miji ya Umbria,
Amatrice, Accumoli na Pescara del Tronto kwa watu kufukiwa kwenye vifusi.
Wakati maafisa wa uokoaji
wakiendelea na juhudi za kuwaokoa watu walionusurika kwenye tukio hilo
walitatizwa na mitetemeko mingine iliyotokea ghafla na kutikisa majumba
yaliyosalia yakiwa bado wima.
Maeneo yaliyokumbwa zaidi na
uharibifu huo ni Accumoli na Pescara del Tronto huku tetemeko hilo likitajwa
kuanzia kwenye Norcia, kilomita 170 kaskazini magharibi mwa mji mkuu Roma.

No comments:
Post a Comment