Harmonize adai Kidogo nachopata kinatosha kumuhudumia Wolper wangu - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 10 August 2016

Harmonize adai Kidogo nachopata kinatosha kumuhudumia Wolper wangu

   1463405234_0653_b
Msanii wa muziki wa label ya WCB, Harmonize amefunguka kwa kusema kuwa kidogo anachokipata katika muziki wake lazima ahakikishe anakula na baby wake ili kulinda status yake.


Muimbaji huyo ambaye anatoka kimapenzi na staa wa filamu, Jacqueline Wolper, amesema gharaza za kumtumza mrembo huyo hazimsumbui kama watu wanavyofikiria.
“Swala la kinywaji vyumbani kwake ana kaunta,so akijisikia kunywa anakunywa nyumbani, mimi nirudi studio namkuta anakunywa, na hajawai kuniambia sijui anatoka na mashoga zake,” Harmonize alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.

Aliongeza, “Mwanamke yupo kwa ajili ya mwanaume anayempenda,so kidogo nachokipata lazima nihakikishe namlinda baby wangu, nalinda status yake.
 Kwa sababu usipo muhudumia mwanamke wako, atamuhudumia nani? atamuhudumia mtu mwingine, so kidogo nachokipata nakitunza kuhakikisha baby wangu anapendeza vizuri na anakula anachokitaka.
 Lakini sidhani kama kuna mwanaume mjinga ambaye anaweza kutelekeza familia yake kwa ajili ya mwanamke, kwa sababu sidhani bila Mama yangu kunizaa na kunituza ningemjua mwanamke, so kwanza Mama yangu alafu inakuja familia yangu, na kwa sababu mwanamke wangu ni sehemu ya familia yangu,”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here