
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mawasiliano
Tanzania (TCRA) imevipa onyo na kuvipiga faini vituo viwili vya televisheni na
kimoja cha redio kwa kukiuka maadili ya utangazaji.
Vituo hivyo ni ITV, Clouds Tv na
Clouds Fm Radio, vyote vya jijini Dar es Salaam, ambavyo kwa ujumla vimepigwa
faini ya Sh milioni 19.
Akitoa uamuzi uliofikiwa na Kamati
ya Maudhui ya TCRA, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joseph Mapunda alisema
vituo hivyo vilibainika kukiuka Kanuni za Huduma za Utangazaji na kuvitaka kuwa
wasimamizi wazuri wa vipindi vyao.
Mapunda alisema kamati hiyo imekipa
onyo na kukipiga faini ya Sh milioni 10 kituo cha televisheni cha ITV kwa
makosa mawili; la kwanza ni kupitia kipindi chake cha Kumekucha cha Juni 15,
mwaka huu kati ya saa 1:00 na 1:30 asubuhi ambacho mtangazaji alifanya
mahojiano na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kuhusu mwenendo wa
Bunge la Bajeti, na Mchungaji Msigwa alitamka maneno ya kashfa dhidi ya Naibu
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.
“…mtangazaji
hakuchukua jitihada za kumwomba Mheshimiwa Peter Msigwa kufuta lugha ya matusi
aliyoitumia, bali alionekana akifurahia na kuendelea kumuuliza maswali
mengine,” alisema Mapunda.
Katika kosa la pili, Mapunda alisema
kituo hicho kilikiuka kanuni katika taarifa ya habari ya Juni 23 kati ya saa
1:00 na 2:00 asubuhi, kilitangaza taarifa ya msichana wa miaka 16 aliyebakwa na
kupewa ujauzito na walitumia utambulisho wa msichana huyo kwa jina na shule
anayosoma.
Katika utetezi wake, Mwakilishi wa
ITV, Stephen Chuwa alikiri kuwa Mchungaji Msigwa alitoa maneno ya kashfa na
hakutembea katika ahadi yake ya kutomkashifu mtu.
Aidha alisema kama mtangazaji
angemuomba kufuta kauli, mjadala ungekuwa mkubwa zaidi. Alisema watachukua
hatua za kumwomba radhi Dk Tulia kutokana na kashfa hiyo.
Kwa upande wa Kituo cha Clouds Tv,
kituo hicho kimepewa onyo na kupigwa faini ya Sh milioni nne ambazo wanapaswa
kulipa ndani ya siku 30 kuanzia siku ya hukumu.
Mapunda alisema kituo hicho kupitia
kipindi chake cha Hip Hop, kilichorushwa kati ya saa 8:00 mchana na 12:00
jioni, kilirusha video ya nyimbo za Asanteni kwa Kuja wa Mwana FA na Break It
Down wa Lil Bebbie, ambazo zinadhalilisha utu wa mwanamke.
Aidha, Clouds Fm pia imepewa onyo na
kupigwa faini ya Sh milioni tano kwa vipindi vyake vya ‘Power Breakfast’ na
Jahazi kwa walikiuka kanuni za utangazaji.
Alisema katika kipindi cha Jahazi
cha Mei 9, kilichorushwa kati ya saa 10:00 hadi 12:55 jioni, watangazaji
walisikika wakishabikia taarifa ya mtu kufanya ngono na mbuzi, ambako walieleza
kuwa mtu huyo na mbuzi ni kama mtu na mpenzi wake, jambo lililoonesha
wanahamasisha vitendo hivyo.
Aidha, Mei 18, mwaka huu katika
kipindi cha Power Breakfast, kilichorushwa kati ya sa 12:00 na 4:00 asubuhi
baada ya kusoma taarifa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhusu kupandikizwa kwa
sehemu za siri za kiume kwa mtoto wa miaka mitatu, aliyezaliwa akiwa hana na
kulelewa kama mtoto wa kike.

No comments:
Post a Comment