Diamond akikadhi hundi kwa uongozi wa GSM
Msanii wa muziki Diamond Platnumz ametoa msaada wa tsh 20 Milioni kwa
‘GSM Foundation’ kwa ajili ya kusaidia jitihada za taasisi hiyo ya kutoa huduma
ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Timu ya Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa na
Upasuaji (MOI) kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikishirikiana na GSM
Foundation imekuwa ikizunguka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya
kutoa huduma hiyo bila gharama yoyote.
Raisi huyo wa label ya ‘WCB’ ameonyesha kughuswa na
jitihada za taasisi hiyo na kuamua kuchangili kiasi hicho.
“Moyo wangu unaniambia nisingeshikwa mkono ama kusaidiwa
na watu basi nami nisingeweza leo hii kufikia hatua hii ndogo niliofikia na
ndio maana kidogo nikipatacho huwa napenda kusaidia wenzangu,” aliandika
Diamond Istagram. “Leo Mapema nilitembelea ofisi za GSM foundation kuwasilisha
kidogo tulichobarikiwa kwa niaba ya WCB. kwajili ya kusaidia watoto wenye
matatizo ya Vichwa vikubwa (Bobble Head Syndrome) na Mgongo wazi,”
Kwa upande wa GSM Foundation, ameandika:Leo tumepokea
hundi ya shilingi milioni ishirini (20,000,000/=) kutoka kwa @diamondplatnumz
kama mchango wake kwa #GSMFoundation. Tunamshukuru kwa kuja kututembelea
ofisini kwetu na kwa msaada aliotupatia. Mwenyezi Mungu amuongezee pale
alipopunguza.

No comments:
Post a Comment