
Leo(Jana) nimewatembelea ndugu zangu wa Kilolo - Iringa kuwashukuru na kuwaeleza kuwa tulishinda na ndio maana hawa mabwana wakubwa wanapata tabu sana Na Sisi.
Miezi michache iliyopita
nilitangaza kuanza ziara ya kushukuru wananchi kwa kura Million 6 wakazuia
mikutano ya hadhara na kama haitoshi wakazuia mikutano ya ndani pia ninayotaka
kuhudhuria ,imefikia mahala wanatisha hadi wafanyabiashara wanaotukodishia
kumbi za mikutano.
CHADEMA chama chetu ni kikubwa sana
, kinawatesa , tumewachapa kweli kweli uchaguzi Mkuu 2015, tumewashinda katika
majiji na miji mikuu kiasi wanapata Tabu , wageni toka Nje wakija pale Airport
Rais huwa anaulizwa kuhusu mameya wetu na anapata kigugumizi kutambulisha kuwa
hawa ni wapinzani.
Ni jambo la kufurahia na sababu ya
sisi kutokata tamaa.
Ni ishara kwamba tunaweza.
Pili Uchaguzi Mkuu ujayo 2020
tutashinda tukiwa wamoja , tuwe wamoja na wanajua sisi ni wamoja . Na nawasihi
tuendelee kuwa wamoja hivi hivi, tusiruhusu vitisho vitutenganishe.. Hakuna
nguvu kubwa kama ya Umma.
Uongozi ni dhamana na njia pekee
njema ya kuongoza ni meza ya makubaliano na sio vitisho kwa wananchi kama
ilivyo sasa.
KUHUSU UKUTA .
Jambo hili la UKUTA ni kubwa mno si
jambo dogo hata kidogo .Jana balozi wa Marekani aliwatumia ujumbe raia wake
wajiandae kuondoka tarehe 1 September kwa hofu walionayo. Hata Mimi nina hofu
kama tusipotekeleza hili nchi itakuwa wapi hapo baadae. Haiwezekani mtu mmoja
ajiamulie tuu kila jambo na kuvunja katiba .
Wasuluhishi wanasema tuzungumze ,
tunakubali kuzungumza ,lakini tuzungumze nini ikiwa mtu anavunja Katiba na
hawamuonyi hawamshauri hii si sawa kabisa.
Mtu mmoja anajiamulia kuvunja
katiba anazuia mikutano anazuia mikutano ya ndani na wasuluhishi hawamuonyi
,nasema kabla ya kuja kwetu wakamueleze yeye kwanza matendo yake .
POLISI niwaeleze duniani kote
maandamano ni haki ya msingi kabisa , police wakiua raia au wanachama wetu
tuwaarifu dhahiri tutagoambana nao mmoja mmoja, hatutahangaika na jeshi
tutahangaika Na Polisi aliefanya mauaji, alie fyatua risasi ajue dhahiri
tutamshitaki ICC .
Ni bora tufilisike ,tutaabike
lakini tutawalinda watanzania Na waandamanaji wetu wote nchi nzima Kata zote
kama tulivyo kubaliana.
Ni aibu vyombo vya dola vinatumia
nguvu kubwa kutisha watu wasio hata na fimbo.
Tabia za baadhi ya viongozi ni
mbovu sana , wanavunja Katiba Na kukanyaga demokrasia , hili hatuwezi
kuliruhusu litokee Tanzania hata kidogo. Zipo jitihada za usuluhishi hatuna
shaka nazo lakini wajue jambo tunalolipigania liko wazi ni Katiba wamwambie aruhusu
mikutano na haki za kidemokrasia .
Tujitokeze kwa wingi sana September
1, tuandamane bila kuharibu Mali ya mtu kama tulivyofanya wakati Wa kuchukua
Fomu pale buguruni ,Tume hadi Kinondoni bila hofu .
Tuna chama Imara sana CHADEMA
kinacho tetea Uhuru ,haki ya mwananchi , maendeleo na ustawi wa nchi .
Tunawapenda sana, ninawapenda Na Ahsanteni.

No comments:
Post a Comment