Jeshi la Polisi kanda
maalumu ya Dar es salaam, limeendelea na mazoezi yake kwaajili ya ukakamavu ili
kujiweka sawa na kupambana na tatizo la uhalifu.
Akiezungumza
na waandishi wa habari Kamishna wa polisi kanda ya Dar es salaam, Simon Siro,
aliwatoa hofu wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi na zoezi hilo kwani halipo
kwaajili ya kuwatisha bali lengo ni kupambana na wahalifu na majambazi.
“Eeh kimsingi ni mazoezi ambayo tunayafanya kupitia maeneo
mbalimbali kwa maana kwamba lengo kubwa ni kuzuia uhalifu hilo ndo lengo la
kwanza, la pili ni kupambana na uhalifu kwasababu tunapokuwa tunapita maeneo
mbalimbali lolote linaweza kujitokeza, wahalifu wanaweza jitokeza”, alisema
kamanda Siro.
Aliongeza kwa kutoa mfano wa matukio yaliowahi kutokea alisema,
“matukio mengi unaweza kuona kama ya panya rodi yanatokea sana sana maeneo ya
Mbagala, lakini tukaona kwanini tufanye mazoezi haya kimya kimya ni vizuri
wananchi wa kaona jeshi lao wakaona ukakamavu wa askari wao.”
“Hata miaka ya nyuma tulikuwa tunafanya na wala hatuna nia mbaya
kabisa kwamba tunatisha wananchi hapana hatuna lengo la kutisha tunafanya
katika mazoezi yetu ya kawaida na lengo kubwa kuzuia uharifu kwenye maeneo
kwasababu naamini mtu muharifu akiona polisi anapita anakimbia”, aliongeza .
Naye kamishna wa oparesheni wa mafunzo ya jeshi la polisi Nsato
Nsazya, aliwataka wananchi wasikejeli mazoezi hayo na kusema hatua kali
zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kufanya hivyo kwa njia mbalimbali ikiwemo
kupitia mitandao ya kijamii.
BY: EMMY MWAIPOPO

No comments:
Post a Comment