Mkurugenzi wa Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu amesema mmiliki wa jengo la Club ya
Bilicanas, Freeman Mbowe ni miongoni mwa wadaiwa sugu wa shirika hilo waliopewa
notisi inayoishia mwezi huu.
Akizungumza
ofisini kwake Dar es Salaam, Mchechu amesema Mbowe anadaiwa malimbikizo ya
kodi.
Hata hivyo amesema suala hilo halina uhusiano na siasa za Ukuta
kwani mbali na Mbowe zipo taasisi na watu binafsi wanaodaiwa.
“Zipo pia taasisi za serikali zikiwemo wizara na idara ambazo
mwezi zitatimuliwa kwenye majengo wanayotumia,” alisema afisa huyo.
Source: Mwananchi

No comments:
Post a Comment