Nandy ameamua kumchukua Mr Blue kwaajili ya remix ya ngoma yake, Nagusa
Gusa.
Amesema ameamua kuja remix ili kutafuta ladha tofauti.
Akiongea kwenye kipindi cha Extra Fleva cha Uplands Fm – Njombe kinachoendeshwa
na Ergon Elly,Nandy alisema awali kwenye wimbo huo alitakiwa kumshirikisha
msanii lakini kwa kuhohofia maneno ya watu kuwa amebebwa, ilibidi autoe akiwa
mwenyewe.
Ameongeza kuwa remix imechangamka
zaidi na baada ya Fiesta watashoot video yake.

No comments:
Post a Comment