Kambi tiba
inayoendeshwa na Taasisi ya Mifupa na upasuaji ya Muhimbili (MOI) kwa ufadhili
wa GSM
Foundation inayojaribu kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na vichwa
vikubwa na mgongo wazi Jumanne hii imeanza kazi Mkoani Iringa, huu ukiwa ni
mkoa wa nne tangu msimu wa pili wa ziara yake ya kuzunguka nchi nzima kuanza.
Kaimu
mkuu wa kambi tiba hiyo, Daktari Bingwa Hamis Shaaban kutoka MOI amesema
kumekuwa na hamasa ndogo kwa wazazi kuleta watoto wao kwa ajili ya tiba hii ya
bure katika msimu huu, ukilinganisha na msimu wa kwanza ambapo jumla ya watoto
101 walifanyiwa upasuaji.
Katika
awamu hii ya pili, mpaka leo hii ni watoto 35 wamefanyiwa, huku ukiwa ni mkoa
wa mwisho kwa kambi hii kupita, hali inayoleta ukweli kwamba inaweza kumalizika
bila kufikia lengo la kutibu watoto 100 na zaidi kama ilivyokuwa awamu ya
kwanza.
Afisa
habari wa GSM Foundation, Bw Khalphan Kiwamba, `Kiwadinho’, amesema sababu kuu
ni wagonjwa kuwa mbali na eneo ambapo tiba inafanyika, na kambi haikuweza
kusogea zaidi kwa sababu za kiufundi kwani upasuaji wa watoto hawa unahitaji
maabara za kisasa ambazo zinapatikana katika Hospitali za mikoa tu.
Kiwamba
kwa upande wake amewaomba wakazi wa iringa kujitahidi kupashana habari ili
watoto wengi wapate kupata tiba hii iliyofadhiliwa tayari.
Kambi
tiba ya GSM kwa msimu huu wa pili inamalizika Agosti 18 mwaka huu wa 2016,
ambapo baada ya tathmini, tarehe za msimu wa tatu zitatangazwa.

No comments:
Post a Comment