Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kuwachukulia hatua wasanii wa Kundi la Orijino Komedi kwa kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za polisi.
Akiongea na Clouds FM Msemaji wa Polisi, Advera Bulimba
ameeleza kuwa wanatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia
mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na majeshi ya ulinzi na usalama hapa
nchini na atakayebainika hawatasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yake.
“Jeshi la Polisi linawashikilia wasanii wa Kikundi cha
Orijino Komedi kwa kuvaa sere za polisi, hilo moja kwa moja ni kosa kisheria na
tayari Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limechukua hatua ya
kuwakamata baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria wasanii hao
watafikishwa Mahakamani. Kufanya hivyo ni kosa, na watuhumiwa wanatakiwa
washughulikiwe kwa mujibu wa sheria za nchi yetu,” alisema Advera.
Wasanii hao wa Kundi la Orijino Komedi walivaa sare hizo
katika harusi ya mchekeshaji mwezano Masanja Mkandanizaji.

No comments:
Post a Comment