Shirikisho la soka nchini (TFF) limetangaza kuwa fedha zitakazopatikana
kwenye mechi ya Ngao ya Jamii zitatumika kuchangia kwenye ununuzi wa madawati
kwa shule ambazo zina uhaba huo.
Mchezo huo unaotarajiwa kufanyika leo kwa kuzikutanisha
timu mbili za jiji moja kati ya Yanga dhidi ya Azam FC kwenye uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya ligi kuu Tanzania Bara kuanza hivi
karibuni.
Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema, “TFF
haijalenga kupata mapato ya kesho “kwenye Ngao ya Jamii kwaajili ya mpango
wowote wa maendeleo ya shirikisho.”
“Tumelenga kuisaidia na kuipa support serikali katika
mpango wake wa kusambaza madawati kwa shule za msingi ili wanafunzi wasikae
tena chini. Kwa upande wetu TFF tunatoa madawati 200,” ameongeza.

No comments:
Post a Comment