Kambi tiba ya upasuaji
wa watoto mwenye vichwa vikubwa na mgongo wazi iliyokuwa imeingia katika msimu
wake wa pili tangu Agosti mosi mwaka huu, imefungwa rasmi mkoani Iringa, huku
watoto 37 wakiwa wamefanyiwa upasuaji.
Dk
Mwanaabas Sued kutoka Taasisi ya MOI, akiongea na wanahabari(Hawapo pichani),
huku akishuhudiwa na Afisa Miradi kutoka GSM Foundation Kibwana Matukio(wa
Kwanza kushoto) Dk John Mtei kutoka MOI,(wa Pili kutoka kulia) na Mkuu wa
Wilaya ya Iringa Richard Kasesela (kushoto)
Aidha, watoto zaidi ya 300 wakipata ushauri nasaha
kutokana na afya zao kutoruhusu kufanyiwa upasuaji.
Awali akiongea kabla hajamkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Bi
Amina Masenza kuongea, Msemaji wa Taasisi ya GSM, Khalfan Kiwamba alisema kila
kukicha wanashukuru kuona maisha ya watoto ambao ilikuwa wapate mtindio wa
ubongo ama kupoteza maisha yanaokolewa kupitia mchango wao pamoja na madaktari
kutoka Taasisi ya ya Mifupa na upasuaji ya Muhimbili, MOI.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, akimjulia hali mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji na
mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji na Kambi tiba ya GSM Foundation.
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI kwa mwaka 2002,
unasema zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na vichwa vikubwa na
migongo wazi, na kati yao ni 500 tu wanaoweza kufika hospitali na kupata
matibabu kutokana na changamoto kuu tatu.
Ya kwanza ni uhaba wa madaktari bingwa wa upasuaji wa
vichwa vikubwa na vikubwa na migongo wazi ambapo kwa tanzania nzima, kwa sasa
wamebaki saba tu, huku sita wakiwa ni waajiriwa wa Taasisi ya MOI na mmoja
akiwa hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza.
Kutokana na uhaba huo wa madaktari, ambao wanapatikana
katika mikoa miwili tu ya Tanzania, Mikoa mingine ambayo watoto wa aina hii
huzaliwa wagonjwa hupata changamoto ya pili ya kusafiri kwenda Dar es Salaam
kwa ajili ya matibabu ambapo hata hivyo, wakifika huko hupata changamoto ya
kukuta foleni ya wagonjwa kutoka mikoa mingine wanaokuwepo kutoka mikoa
mingine.
Kuna imani pia za kishirikina ambapo watoto wengi
hupelekwa kwa waganga, wakihisi labda wamelogwa, wakati hili ni tatizo la
kiafya ambalo mtoto akiwahishwa anaweza akawahishwa hospitali na akapona.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa, Bi Amina Masenza
amewaomba GSM Foundation warudi tena Iringa kwani anahisi wagonjwa waliotibiwa
kutoka mkoa wake ni wachache sana, ukilinganisha na idadi anayoijua ya watoto
waliomo mkoani humo.
Mkuu huyo ametoa maagizo kwa wakuu wa wilaya kuhakikisha
kwamba wanajua idadi ya wagonjwa waliomo katika wilaya zao ili waeze
kuwatayarisha kwa ajili ya matibabu kabla hajawasiliana na wataalamu ili
kulimaliza tatizo hilo kama sio kulimaliza kabisa.

No comments:
Post a Comment