Msanii wa muziki, Snura Mushi ameeleza jinsi anavyosumbuliwa na wanaume
kutokana na uchezaji wake akiwa stejini.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo
‘Shindu’, amesema licha ya kupata usumbufu huo kwa wanaume hao lakini amekuwa
akijitunza na kujiheshimu kwani anafanya hivyo kulinda kazi yake na heshima
yake kama mwanamke.
“Unajua watu wakisikia Snura Chura huwa wanatokea wengi
sana, na kweli huwa napata shida sana kwa wanaume wengi wenye matamanio,” Snura
alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA. “Na inawezekana kweli kati yao wapo
wenye mapenzi ya kweli na mimi lakini ndiyo hivyo,”
Aliongeza, “Kitu nachozingatia sana ni kuilinda kazi
yangu, hivyo wanapotokea wanaume wa namna hii mimi nachokifanya siku zote ni
kuwa mbali nao kabisa ndiyo maana nashinda vishawishi hivyo kila siku” alisema
Snura
Muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii wa kike ambao
wanatumia viuno kuwapagawisha mashabiki wake akiwa stejini.

No comments:
Post a Comment