Tangu malkia wa filamu
nchini, Wema Sepetu aachane na mpenzi wake Idris Sutlan kuna mengi yamekuwa
yakizungumzwa katika mitandao ya kijamii.
Muigizaji
huyo hakuwahi kuzungumza sababu ya kuachana na mshindi huyo wa shindano la Big
Brother Africa Hotshots 2014 hali ambayo imekuwa ikiibua maswali mengi kwa
mashabiki wake.
Alhamisi
hii Wema amewataka mashabiki wake katika mitandao ya kijamii kukaa mkao wa kula
kwa ajili ya kuyasikia mengi ambayo yanaukabili moyo wake.
“Kuna
muda mtu unaweza ukakaa na ukasema na moyo wako, Ila moyo mara nyingi huwa
unazidi nguvu nyingine zozote. Kuna kitu kiukweli ninacho kwa moyo wangu,”
aliandika mwigizaji huyo kupitia ukurasa wa instagram.
Aliongeza,
“Lakini siwezi kusema leo wala kesho, but ipo siku isiyo na jina wala tarehe
nitakisema tu, maana mnanijua kukalfisha nafsi huwa sipendi, but all in all
tuseme Inshallah,”
Wiki
iliyopita aliyekuwa mpenzi wake, Idris Sultan aliamua kufuta akaunti yake ya
instagram yenye followers zaidi ya milioni 1 baada ya kushindwa kuvumilia yale
yanayoendelea katika mitandao ya kijamii.

No comments:
Post a Comment