Q Chief amethibitisha
nyumba yake kuvamiwa na majambazi na wamefanikiwa kuiba baadhi ya vitu
vilivyomo ndani ikiwemo laptop iliyokuwa na baadhi ya colabo zake.
Akiongea
na Clouds FM, muimbaji huyo amedai kuwa thamani ya vitu vyake vilivyoibiwa ni
kama milioni mbili au tatu.
“Watumishi
wa shetani wameamua kufanya kitu cha kihistoria, siku zote wanarukaruka mmoja
wawili tunapigiza nao kelele wanaondoka lakini this time wamekuja watu kama
sita, saba au nane.
Wamekuja na mapanga, wamekuja na mafokolisti yale ya
kufungua, wamekuja na gari moja nje sasa sijui walikuwa wanataka kubeba kila
kitu?,” ameuliza Q Chief.

No comments:
Post a Comment