
Rapper Nay wa Mitego amedai
ametimiza matakwa aliyopewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) baada ya
kufungiwa kwa wimbo wake wa ‘Pale Kati’, ambapo Jumatano hii taachia version ya
kwanza ya video ya wimbo huo.
Nay amewataka mashabiki wake wa
muziki wa kimataifa kukaa mkao wa kula.
“Mimi na BASATA tulishamalizana,
wao walinipa maazimio na mimi nimeshayatekeleza, kwa hiyo na mimi naendelea na
issue zingine,”alisema Nay.
“Jumatano hii mashabiki wangu
Wakimataifa pamoja na wa kwenye mitandao ya kijamii wakae mkao wa kula, naachia
video,”
Rapper huyo alisema wimbo wa ‘Pale
Kati’ una nguvu kubwa sana na unafanya vizuri katika baadhi ya nchi kama Kenya,
Uganda pamoja na Ghana, na ndio maana ameamua kuanza kutoa video kwa ajili ya
kimataifa kwanza.
Pia amewataka mashabiki wa muziki
wake kuendelea kusubiria mambo mazuri kwani wimbo huo una video nne.

No comments:
Post a Comment