Msanii wa muziki, Linex Sunday Mteja amesema mradi wake wa kuwaandikia
watu nyimbo ndiyo mradi pekee kwenye muziki wake ambao unampatia pesa za
uhakika.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Linex amesema anaweza
kujipa mapumziko kwenye muziki na kuishi maisha mazuri kwa kutegemea pesa za
kuwaandikia watu nyimbo.
“Bado nawaandikia watu nyimbo, tena ni mchongo ambao
unanipatia pesa nyingi sana,” alisema Linex. “Yaani naweza hata nikapumzika
kufanya show nikawa nategemea pesa za kuwaandikia watu nyimbo, kwa hiyo ni kitu
ambacho kinanipiga tafu sana, naishi bila hata stress,”
Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Hewala’,
amesema wanandoa ni moja kati ya wateja wake wakubwa katika mradi huyo.
Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa
kula kwa ajili ya ujio wa video yake mpya ya wimbo ‘Hewala’.

No comments:
Post a Comment