Baada ya hivi karibuni Mzee Yusuf kutangaza kuachana na kufanya muziki,
ameweka wazi kuwa kilimo na ufugaji ndiyo kimbilio lake.
Muimbaji huyo mahiri wa taarab alitangaza azma hiyo
Ijumaa iliyopita kwenye msikiti wa Taqwah jijini Dar es Salaam huku akidai kuwa
kuanzia sasa atakuwa akimtumikia Mungu zaidi.
Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, Mzee
Yusuf amesema baada ya kuachana na kufanya muziki anaenda kujikita na kilimo
pamoja na ufugaji.
“Nimeacha kwa ridhaa yangu mwenyewe,” alisema Mzee
Yusuf. “Ni mimi mwenyewe nilikaa nikaamua niachane na muziki nitafute vitu vya
halali nifanye ili niwe nafanya ibada vizuri,”
“Kwa sababu nilikuwa naswali lakini nahofu, kwa sababu
muziki ni haramu. Kwa hiyo sasa hivi nitafanya biashara nyingine, nitakuwa
nafuga, nimeanza pia kulima, kwa ufupi nitakuwa mkulima,” aliongeza.
Wimbo wa mwisho alioutoa Mzee Yusuf ulikuwa Hewallah
aliomshirikisha Vanessa Mdee.

No comments:
Post a Comment