
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa
ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA jana alitembelea shule ya Nanja
iliyoungua moto hivi karibuni mkoani Arusha.
Akiambatana na viongozi wengine
katika jimbo la Monduli Lowassa aliwataka viongozi kuhakikisha shule za bweni
zinajengwa vizuri na kuwekewa mifumo ya kujikinga na ajali za moto kama ambavyo
sasa shule tano kwa kipindi kifupi zimeungua moto mkoani Arusha na chanzo
kikiwa hakijulikani.
“Napenda kuwakumbusha wakuu wa
shule na viongozi kwamba ni muhimu shule zote za mabweni ziwezeshwe na zijengwe
vizuri huku zikichukuliwa tahadhari zote za kujikinga na ajali kama hizi, pia
nitaungana na uongozi wa jimbo la Monduli pamoja na wadau mbalimbali
kuhakikisha shule hii inarekebishwa na watoto wanarejea katika mabweni” Alisema Lowassa.
Aidha Lowassa alitumia nafasi hiyo
kuwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii kwani elimu ndiyo mkombozi wa maisha yao.

No comments:
Post a Comment