Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imewaonya watumiaji wa mitandao ya
kijamii wanaojisajili katika mitandao hiyo kwa kutumia majina na taarifa za uongo.
Kaimu Mkurugenzi wa TCRA, James Kilaba ameyasema hayo
Jumatano hii, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi
sahihi na salama ya mitandao ambayo inasimamiwa na kitengo cha dharura cha
kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao hapa nchini (TZ-CERT).
Kilaba amesema, vitendo vya watu kujisajili katika
mitandao ya kijamii kwa kutumia majina na taarifa zisizo sahihi, ni kosa
kisheria na kwamba wanaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
“Tumeamua kuzindua kampeni hii ili kuwasaidia wananchi
kuepuka makosa ya kimtandao na kuepuka kufanyiwa utapeli au wizi mitandaoni kwa
sababu matukio mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa au kulalamikiwa yanazuilika
kwa watu kupewa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao,” alisema Kilaba.
Pia Kilaba alitoa ufafanuzi jinsi ya kutoa elimu hiyo
kampeni hiyo ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao,
itafanyika kupitia matangazo ya redio, televisheni, magazeti pamoja na mitandao
ya kijamii ambapo katika mitandao ya kijamii itajulikana kama, “Darasa
mtandao”.
“Miongoni mwa mambo ambayo tutawafundisha wananchi ni
kutoweka wazi taarifa zao binafsi zote katika mitandao, kubadili na kutunza
neno la siri (password), kutojibu ujumbe unaosema umeshinda bahati nasibu na
menginey

No comments:
Post a Comment