
Viongozi waandamizi wa Chadema
akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana walikamatwa na Jeshi la
Polisi wakati wakiwa katika kikao cha ndani katika Hoteli ya Giraffe mkoani Dar
es Salam.
Lowassa, ambaye alikaa kituoni hapo kwa takribani saa tatu anaweza kuwa kiongozi wa kwanza aliyewahi kushika nafasi ya Waziri Mkuu kuhojiwa na polisi.
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu
Lissu aliwataja viongozi wengine waliokamatwa kuwa ni Mwenyekiti, Freeman
Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika na
Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa.
Mara baada ya kukamatwa, walipelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi ambako baadhi ya wajumbe na wabunge waliwafuata na kuwasubiri nje ya kituo hicho kujua hatima yao.
Mara baada ya kukamatwa, walipelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi ambako baadhi ya wajumbe na wabunge waliwafuata na kuwasubiri nje ya kituo hicho kujua hatima yao.
Viongozi hao walionekana wakiingia
Polisi saa 10.30 jioni na kutoka saa 1.25 usiku, jambo ambalo liliwafanya wakae
kituoni hapo kwa saa tatu.
Lissu alisema polisi walivamia
kikao hicho kilichokuwa na wajumbe 170, wakiwamo baadhi ya wabunge wa chama
hicho na kuwakamata viongozi hao kwa maelezo kuwa wamekaidi amri ya Jeshi la
Polisi ya kuzuia mikutano ya ndani na nje ya vyama vya siasa.
Imeelezwa kuwa viongozi hao wa
Chadema walikuwa na mkutano uliotanguliwa na kikao cha viongozi wakuu na kufuatiwa
na cha viongozi hao kikijumuisha wabunge, mameya na wenyeviti wa
halmashauri.
Wakiwa katika kikao hicho,
ilielezwa kuwa watu wanne waliingia wakiwa wamevalia kiraia na kuwaeleza kuwa
viongozi wao wanahitajika kituo kikuu cha polisi kutokana na kufanya mkutano
kinyume cha sheria.
Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo
Peneza ambaye alikuwa kwenye mkutano huo alisema pamoja na mambo mengine
ya chama, walikuwa wakijadili suala la operesheni Ukuta la Septemba Mosi kama
liendelee au lisiendelee kutokana na hali ilivyo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwao, alisema viongozi
hao walikamatwa kwa kukukaidi amri ya polisi ya kuzuia mikusanyiko ya
kisiasa na kuchochea wananchi kuandamana kinyume cha sheria Septemba
Mosi.
Alisema baada ya kuachiwa kwa dhamana, viongozi hao wametakiwa kuripoti kituoni hapo leo.
Alisema baada ya kuachiwa kwa dhamana, viongozi hao wametakiwa kuripoti kituoni hapo leo.
Wiki iliyopita, Jeshi la Polisi
kupitia kwa Kamishana wa Operesheni na Mafunzo, Nsato Marijani lilipiga
marufuku mikutano ya ndani likisema inatumika kuhamasisha watu kuvunja sheria
za nchi na kupambana na askari.
Hatua hiyo ilikuja huku jeshi hilo likiwa limepiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano kufuatia uamuzi wa Rais John Magufuli kuzuia shughuli za kisiasa hadi 2020.
Hatua hiyo ilikuja huku jeshi hilo likiwa limepiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano kufuatia uamuzi wa Rais John Magufuli kuzuia shughuli za kisiasa hadi 2020.

No comments:
Post a Comment