
Madiwani watatu wa Chadema na mfuasi mmoja wa chama hicho
wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Rombo kwa makosa ya kufanya
uchochezi.
Madiwani hao, Nicolaus Kimario (Kirio), Anasia Kimario (Viti
Maalumu), Daud Tarimo (Leto ) na mfuasi wa Chadema, Rogath Kanje walikana
mashtaka hayo.
Mwendesha mashtaka, Bernard Machivya alieleza mahakama kuwa
washtakiwa walitenda kosa hilo Agosti 25, wakiwa nyumbani kwa mmoja wa
washtakiwa Nicolaus Kimario.
Aliieleza Mahakama kuwa washtakiwa wote wanne walitenda kosa
hilo kwa pamoja wakifanya vikao vya kuhamasisha wananchi wajitokeze kwenye
maandamano ya Ukuta Septemba Mosi.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Rombo, Naomi Mwerinde
aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 5 na watuhumiwa wote wataendelea kukaa
rumande.

No comments:
Post a Comment