
Upande wa Jamhuri katika kesi
inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na wahariri wa
Gazeti la Mawio iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu umeshindwa
kuwasomea washtakiwa hao mashtaka mapya baada ya wakili anayewatetea, Peter
Kibatala kudai kuwa yaliyofutwa yamerudishwa kwa ‘staili’ tofauti.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya
Kibatala kuwasilisha hoja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba za kupinga
washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo mapya.
Wakili wa Serikali Mkuu, Kishenyi
Mutalemwa aliwasilisha maombi mahakamani hapo akiomba kuwasomea hati mpya ya
mashtaka washtakiwa hao na Mahakama iliipokea na kuruhusu isomwe, lakini Wakili
Kibatala alipinga kwa madai kuwa hayatofautiani na yale yaliyofutwa Juni 28,
2016.
Kibatala alidai katika hati mpya
shtaka la kwanza na la tano ni sawa na yale yaliyokuwamo kwenye hati iliyofutwa
mahakamani hapo baada ya kupingwa na kuonekana hayakustahili kwa mujibu wa
sheria.
Baada ya Kibatala kuwasilisha hoja
hizo, Wakili Kishenyi aliiomba Mahakama hiyo kuiahirisha kesi hiyo kwa muda ili
aweze kujibu hoja zilizotolewa na upande wa utetezi na hakimu aliridhia na
kuiahirisha hadi saa sita mchana.
Ilipofika mchana, Kishenyi alidai
shtaka la kwanza na la tano ni kama hayakuwapo mahakamani na kwamba kufutwa
kwake haikatazwi kuyarudisha tena na mashtaka hayo ya awali yalifunguliwa bila
ya kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), lakini hivi sasa
yamerudishwa yakiwa na kibali hicho.
Kuhusu kukata rufaa, Kishenyi
alidai wanakata rufaa kwenye kesi ambayo ilisikilizwa na kumalizika. Baada ya
kusikiliza hoja za pande zote, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo na kuwa
atatoa uamuzi wa hoja hizo mwezi ujao.
Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi
hiyo ni Mhariri wa gazeti hilo, Simon Mkina, Jabir Idrisa, Mchapishaji wa
Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob na Lissu ambao kwa pamoja walikuwa
wanakabiliwa na mashtaka matano yakiwamo ya kuandika habari za uchochezi
kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002

No comments:
Post a Comment