
Mahabusu aliyekuwa akishikiliwa
katika kituo kikuu cha polisi jijini Arusha aliyetambulika kwa jina la Victoria
Wenga (51) mkazi wa Lemara jijini Arusha amejinyonga hadi kufa usiku wa kuamkia
jana kwa kutumia shuka lake bila kuacha ujumbe wowote.
Marehemu alikamatwa Agosti 21 mwaka
huu majira ya Alfajiri kwa tuhuma za kuchoma moto nyumba yake na maduka yake
mawili kutokana na ugomvi wa kifamilia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,
Charles Mkumbo alikiri kutokea kwa tukio hilo katika Kituo cha Kikuu cha Polisi
saa 6:20 usiku jana wakati wenzake wakiwa wamelala.
“Polisi wa zamu
alisikia kelele kutoka kwenye chumba cha mahabusu wa kike ambapo polisi
walijitahidi kuokoa maisha ya mahabusu huyo, lakini ilishindikanika,” alisema
Kamanda Mkumbo.
Mahabusu huyo, ambaye ni mkazi wa
Lemara jijini Arusha, alijinyonga kwa kutumia shuka lake alilokuwa anatumia
kujifunikia wakati yuko mahabusi. Mtuhumiwa huyo, alijinyonga kabla ya
kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yake.
“Jana ilikuwa
afikishwe mahakamani kujibu kosa lililokuwa linamkabili,”alisema Kamanda
Mkumbo na kuwahakikishia kuwa hali ya usalama kituoni hapo na tukio hilo,
havihusiani na sababu zozote za kiusalama.
Marehemu Victoria anadaiwa kuwa na
ugomvi wa kifamilia na mume wake aliyetambulika kwa jina la Edward Wenga
akimtuhumu kuzaa nje ya ndoa kinyume na utaratibu.
Imeelezwa kuwa hicho ndo
chanzo cha marehemu kufikia hatua ya kuteketeza mali walizochuma na mume wake
ambazo ni maduka mawili na nyumba ya kuishi.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa
katika chumba cha kuifadhia mahiti Hospitali ya Mount Meru.

No comments:
Post a Comment