Ukiona kwako kuna fuka moshi jua kwa mwenzako kunaungua. Hilo ndio
linalotokea kwenye soka la bongo kwenye timu za Simba na Yanga ni kama sinema
ya kihindi.
Habari ya Yusuf Manji kujiuzulu kwenye nafasi yake ya
uenyekiti ndani ya klabu ya Yanga ndio imekuwa stori kubwa ikiwa ni siku chache
tangu atangaze kutaka kuikodi timu hiyo kwa muda wa miaka kumi.
Manji alifikia maamuzi hayo baada ya kuona kuwa
anashutumiwa vibaya na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali na
viongozi wengine wa Yanga na kumpelekea kukaa pembeni ili kulinda heshima yake.
Kitendo hicho kimepokelewa kwa huzuni na jaziba na
mashabiki pamoja na wanachama wa timu hiyo Jumanne hii ya Agosti, 17 walikutana
katika makao makuu ya klabu yao na kukubaliana kumsimamisha uanachama Katibu
Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali ambaye alidaiwa ndiyo
aliyechochea Manji kuchukua uamuzi huo baada ya kuzungumza katika vyombo vya
habari kuwa Manji amekurupuka.
Baada ya hayo yote, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari
wa Yanga aliyefungiwa na TFF, Jerry Muro ametoa taarifa kutoka kwa Manji ambayo
amemwagiza aifikishe kwa mashabiki wa klabu hiyo inayozungumzia hatma ya
mahusiano yake na Yanga.
“Jerry waambie wana Yanga
pamoja na vurugu zote hizi nitaendelea kuwa upande wao na kamwe sitawaacha
nguvu yangu iko kwa wanachama,wapenzi na mashabiki”-Bw Yusuf manji,” ujumbe wa Manji kwa mashabiki wa Yanga.

No comments:
Post a Comment