Rais Magufuli ambaye
aliongozana na mkewe Mama Janeth, pia kumtembelea na kumjulia hali Spika wa
Bunge, Job Ndugai aliyerejea hivi karibuni akitokea India alikokwenda kuangalia
afya yake.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Bi Janeth akifanya maombi ya pamoja
“Kiukweli
nimefarijika sana nimshukuru mheshimiwa Rais kwa kuja kunitembelea na Mungu
ambariki, hata kipindi nikiwa hapa nchini alikuwa akinijulia hali hata pia
nilivyokuwa nimesafiri kwenda India amekuwa akinipigia simu mara kwa mara na
nashukuru amekuja kwa niaba ya Watanzania, na pia niwahakikishie Watanzania
kuwa naendelea vizuri, tuzidi kuombeana”,alisema Ndungai.
Naye
John Malecela alisema “namshukuru Rais Magufuli pamoja na madaktari
wanaonipatia matibabu, na pia hali yangu kwa sasa ni nzuri.”.
“Nawaombea
kwa mwenyezi Mungu wapone na kupata nguvu haraka ili waweze kuendelea na
majukumu yao kawaida ya ujenzi wa taifa,” alisema Rais Magufuli.
BY:
EMMY MWAIPOPO

No comments:
Post a Comment