Mwanandondi
Manny Pacquiao anatarajia kulejea ulingoni mnamo tarehe 5 Novemba kukabiliana
na bingwa wa dunia wa uzani wa welter Jessie Vargas kutoka Marekani.
Pacquiao,
37, bingwa wa zamani wa dunia, ametangaza kwamba atarejea licha yake kutangaza
kwamba angestaafu baada ya kumshinda Timothy Bradley mwezi Aprili.
Promota
wake Bob Arum alisema mwezi uliopita kwamba mwanabondia huyo kutoka Ufilipino
angepigana tena mwaka huu.
“Maisha ya kustaafu hayamfai Manny kwa sasa,” meneja wa Pacquiao Michael Koncz aliambia gazeti la Los Angeles Times.
“Ndondi zimo kwenye damu yake.”
“Maisha ya kustaafu hayamfai Manny kwa sasa,” meneja wa Pacquiao Michael Koncz aliambia gazeti la Los Angeles Times.
“Ndondi zimo kwenye damu yake.”
Pacquiao
na kundi lake watakutana 10 Agosti mjini Manila kuamua iwapo pambano hilo dhidi
ya Vargas, 27, litaandaliwa Los Angeles au Dubai.
Vargas
alitwaa ubingwa mwezi Machi baada ya kushinda raia mwenzake Sadam Ali.
No comments:
Post a Comment