Meneja wa mwanamuziki wa kimataifa
Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kwa jina la ‘Babu Tale’ hivi sasa
yupo mikononi mwa polisi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Babu Tale amekamatwa leo na
kufikishwa mahakamani hapo ili ajieleze ni kwa nini asifungwe kwa kushindwa
kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250 milioni kwa
makosa ya kuvunja sheria ya Hakimiliki.
Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo
kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza
nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume
na haki miliki.
No comments:
Post a Comment