
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro, Agnes Mkandya amemwaga machozi alipokuwa akiulizwa maswali na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).
Tukio hilo lilitokea jana wilayani
humo baada ya kamati hiyo kumuuliza Mkurugenzi huyo maswali mbalimbali ikiwa ni
pamoja na udanganyifu na ubadhirifu wa fedha mkubwa unaoonekana kufanywa na
baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo.
Swali lililomliza Mkurugenzi huyo
liliulizwa na Mbunge wa viti maalum, Leah Komanya (CCM), aliyetaka majibu
kuhusu wizi wa mapato kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumia karatasi
maalum, unaofanywa na watendaji hao.
Mkurugenzi huyo alikiri kuwepo
ubadhirifu mkubwa wa fedha ndani ya Halmashauri hiyo na kueleza hatua
alizochukua, huku akijitetea kuwa yeye ni mgeni hivyo mambo mengi bado
hajayafanyia kazi.
“Kamati ielewe kwanza Halmashauri
ya Gairo imeoza na ni chafu kwa sababu kuna ubadhirifu mkubwa. Tayari
nimewasimamisha kazi watumishi tisa wa idara, lakini kumbukeni na mimi ni mgeni
sina muda mrefu,” alijibu
Mkurugenzi huyo kabla ya kuanza kumwaga chozi.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa
na mwenyekiti wake, Vedastus Ngombale Mwiru walimtuliza kwa kumbembeleza wakimtaka
aondoe woga kwani ni maswali ya kawaida aliyoulizwa.
Baada ya hali hiyo, Mwenyekiti huyo
aliamuru majibu ya maswali hayo na mengine kutolewa na Mkaguzi wa Ndani wa
Halmashauri hiyo kwakuwa yeye alikuwepo muda mrefu.

No comments:
Post a Comment