Rapper Nay wa Mitego amefunguka na kuzungumza madai ya kugombana na
kuachana na mtayarishaji wake mahiri wa studio yake ya Free Nation, Mr Ttouch.
Wawili hao kwa sasa kila mmoja anafanya kazi kivyake
baada ya kudaiwa kuhitilafiana kwenye masuwala ya pesa.
Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Nay wa Mitego amesema
yeye hajagombana na Mr Ttouch kama baadhi ya watu wanavyosema.
“Mimi kwangu namchukulia Mr T kama mtoto aliyekuwa
nyumbani na sasa amekuwa mtu mzima anaamua kutafuta maisha yake, kwa hiyo mimi
namtakia mafanikio mema katika maisha yake,” alisema Nay.
“Mimi ndiye niliyemtafuta Mr T na kuamua kumkabidhi
studio, nikawa sichukui hata shilingi mia, kwa hiyo mimi nachoweza kusema
muache aende kwa sababu amekuwa mtu mzima,” aliongeza.
Pia rapper huyo amesema kwa sasa kama ana kazi
atamtafuta mtayarishi huyo kwa ajili ya kazi lakini hawezi tena kufanya naye
kazi kishkaji kama zamani.

No comments:
Post a Comment