Mwenyekiti wa Bodi ya Parole ambaye
pia ni Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema amemtaka Waziri Mkuu Mstaafu Edward
Lowassa akubali kwamba alishindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na akae
kimya hadi mwaka 2020.
Mrema aliyasema hayo jana Jijini
Dar es Salaam na kusisitiza kwamba alimtaka Waziri Mkuu Mstaafu watoke CCM
pamoja kwa kuwa nguvu ya upinzani ilikuwa kubwa sana.
‘’Mimi nitamuuliza 1995 wakati
natoka nilikuambia tutoke sasa maji yamechemka tukiweka unga tutakula ugali
ukagoma, ukasema unaendelea kula kidogo hadi alipojiuzulu akaendelea na CCM
hadi alipotaka kugombea Urais akakataliwa na wenzake ndipo akaja upinzani’’
Mrema aliongeza kwamba Chama cha
Mapinduzi kilitakiwa kuondoka madarakani mwaka 1995 ambapo yeye ndiye alikuwa
na nguvu kubwa ya kisiasa nchini.
Aidha Mrema amewataka vijana kuwa
makini na upinzania kwa kuwa Lowassa alijiunga na upinzani baada ya kunyimwa
nafasi ya kugombea Urais ndani ya CCM hivyo wajiepushe na maandamano kwani
hayana faida kwao.
No comments:
Post a Comment