Mkazi mmoja wa jijini hapa, Said
Shomari (64) amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela baada ya kupatikana na hatia
ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Shomari ambaye ni fundi saa, alitiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu hiyo na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo baada ya mshtakiwa kukiri kosa hilo.
Alikiri kutenda kosa hilo jana
alipopandishwa kizimbani mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Adolf Mkini
kumsomea mashtaka yaliyokuwa yakimkabili kwa lengo la kumkumbusha, wakati kesi
hiyo ilipoitwa kwa ajili ya usikilizwaji.
Katika kesi hiyo, Shomari
alishtakiwa na mtoto wake, mfanyabiashara Ramadhani Said (40), kwa makosa
mawili, moja la kukutwa na silaha na la pili la kukutwa na risasi bila kibali
na kinyume cha sheria.
Katika mashtaka hayo, Shomari
alikiri kosa moja la kumiliki silaha na akakana kosa la kumiliki risasi kinyume
cha sheria.
Hata hivyo, wakati Shomari akikiri
kutenda kosa hilo moja na kuhukumiwa adhabu hiyo, mtoto wake alikana kutenda
makosa hayo yote.
Awali, akiwasomea mashtaka hayo,
Wakili Mkini alidai kuwa Novemba 9, 2015, eneo la Kigogo, wilayani Ilala,
mshtakiwa alikutwa akimiliki bastola moja ndogo pamoja na risasi moja bila kuwa
na kibali.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo na kuulizwa kama ni kweli au si kweli, ndipo alipokiri kutenda kosa hilo kwa kujibu kuwa ni kweli, hivyo Mahakama ikamtia hatiani.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo na kuulizwa kama ni kweli au si kweli, ndipo alipokiri kutenda kosa hilo kwa kujibu kuwa ni kweli, hivyo Mahakama ikamtia hatiani.
“Kwa kuwa mshtakiwa amekiri kutenda
kosa kwa shtaka linalomkabili, Mahakama inamtia hatiani na kumhukumu adhabu ya
kifungo cha miaka 15 jela.”, alisema hakimu Mashauri.
Baada ya kutoa hukumu hiyo aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 15, mwaka huu, wakati kesi hiyo itakapoendelea kusikilizwa shtaka moja kwa upande wa Shomari na mashtaka yote mawili kwa upande wa Ramadhani.

No comments:
Post a Comment