Wananchi mkoani Geita wametakiwa kuacha tabia ya
kujichukulia sheria kwa kuwapiga mpaka kuwaua watuhumiwa wa uhalifu, hatua
ambayo inaweza kusababisha mauaji ya watu wasio na hatia.
Wito huo umetolewa na familia ya
bwana Marwa Petro mwenye umri wa 22, mkazi wa mtaa wa uwanja kata ya
Kalangalala Wilayani Geita aliyeuawa juzi kwa kupigwa na wananchi kwa kile
kilichodaiwa kuwa alikuwa ni mwizi.
Tukio hilo limetokea Ijumaa
iliyopita kwenye mtaa wa uwanja kata ya Nyankumbu wilayani Geita ambapo bwana
Marwa alivamiwa na waendesha bodaboda akiwa kwa rafiki yake ambapo
alipigwa kwa mawe na marungu mpaka kupoteza maisha.
Mwenyekiti wa mtaa huo, Joseph
Msoma amelaani kitendo hicho cha kikatli na kuwataka wananchi kuacha tabia
kujichukulia sheria mkononi ambapo amesisitiza kwamba kufanya hivyo ni makosa.
Jeshi la polisi Mkoa wa Geita
limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na uchunguzi unaendelea ili kubaini
waliofanya mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment