Kuna habari imesambaa mtandaoni kuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe
amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi wa nchi hiyo Augustine Chihuri kuwakamata
wachezaji wote wa timu iliyokwenda kushiriki michuano ya Olimpiki nchini Brazil.
Inasema Mugabe amechukua hatua hiyo baada ya kuumizwa na
wachezaji hao kushindwa kupata hata medali moja kwenye mashindano hayo huku
pesa iliyowekezwa kwenye timu ili kuiwakilisha nchi ingeweza kutumiwa kununulia
dawa na kujenga shule.
“Jambo hili ni sawa na mwanaume
asiyelijali kuoa wanawake watano, maana yake nini? Nitahakikisha tunagawana
hasara, wote watailipa serikali bila kujali huku wakijua kuwa fedha
zilizowapeleka huko zinatoka kwenye mifuko ya wananchi,” Mugabe anadaiwa
kusema.
“Tumepoteza pesa za taifa kwa ajili
ya hao panya tunaowaita wanamichezo. Kama hauko tayari kujitoa na kushinda japo
medali ya shaba kama wenzetu wa Botswana walivyofanya, sasa kwanini ulienda
kupoteza pesa zetu,” ameongeza.
Cha kuchekesha zaidi, Mugabe
alidaiwa kusema, “kama tulihitaji watu kwenda Brazil kuimba wimbo wetu wa taifa
na kupeperusha bendera, tungewaagiza warembo na vijana watanashati kutoka Chuo
Kikuu cha Zimbabwe wakatuwakilishe.”
Zimbabwe ni miongoni mwa mataifa
ambayo wanamichezo wake hawakufanikiwa kushinda medali ikiwa inawakilishwa na
wanamichezo 31. Mchezaji ambaye alionekana kufanya vizuri ni yule aliyekamata
nafasi ya nane.
Hata hivyo kuna uwezekano habari
hii inaweza kuwa ni ya kutengenezwa (satire) kama nukuu mbalimbali za
kuchekesha ambazo amekuwa akidaiwa kuzisema.

No comments:
Post a Comment