
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva jana alimtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai nyumbani kwake Jijini Dar es Salam
na kumjulia hali baada ya kurejea kutoka nchini India alikokwenda kwa ajili ya
matibabu.
Akiwa nyumbani kwa
spika Jaji Lubuva pia alimkabishi Mh. Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa
Rais Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2015 na kumueleza kuwa kukamilika kwa
ripoti hiyo ndio hitimisho la Uchaguzi Mkuu na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu
ujao.
Kwa upande wake Mheshimiwa Ndugai
aliipongeza hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya kuweka mikakati ya kushiriki
katika maonyesho mbalimbali yakiwemo yale ya biashara SabaSaba na Nanenane
katika kutoa elimu kwa wananchi.
Jaji Mstaafu Lubuva alikwenda
kumjulia hali Ndugai ambaye kipindi cha Bunge la Bajeti lililomalizika
hivi karibuni, alikuwa nchini India kwa matibabu na hivi sasa afya yake
imezidi kuimarika.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva
(kushoto) akimkabidhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh.Job Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka
2015 wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es
Salaam.

No comments:
Post a Comment