
SAED Kubenea Mbunge wa Jimbo la
Ubungo jana alijisalimisha Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
na kuhojiwa kabla ya kupewa dhamana kufuatia tuhuma za kuandika makala
inayodaiwa kuwa ya uchochezi kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar.
Kubenea ambaye anadaiwa kufanya
uchochezi kwa kuandika makala katika gazeti la MwanaHALISI toleo la 349 la
Julai 25-31 yenye kichwa cha habari, ‘Yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar?’
Kubenea alifika katika kituo hicho
cha Polisi jana saa saba na robo mchana (13:15) akiwa na Tundu Lissu
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na
Frederick Kihwelu wakili mwandamizi wa Chama hicho.
Baaada ya kuhojiwa kwa zaidi ya
masaa mawili, saa tisa na robo alasiri (15:45) alitoka na kuondoka huku
wandishi wa habari wakishindwa kuzungumza naye baada Jeshi la Polisi kuwazuia
waandishi wa habari kuingia katika eneo la kituo hicho.
Akizungumza kwa njia ya simu, Lissu
ambaye ndiye mwanasheria wa Kubenea katika sakata hilo alisema kuwa, Kubenea
amehojiwa kwa madai ya uchochezi lakini alichokiandika ni hali halisi ya
Zanzibar hususani visiwa vya Pemba.
“Kubenea amechiwa kwa dhamana na
ameamriwa kurudi tena kituoni hapo tarehe 18 Agosti, mwaka huu,” alisema
Lissu.
Katika makala yake inayodaiwa kuwa
ni ya kichochezi iliyokuwa na kichwa cha habari, “Yuko wapi
atakayeiokoa Zanzibar?” Kubenea alielezea jinsi Jeshi Polisi Visiwani
Pemba wavyonadaiwa kuwabambikia kesi wananchi, kuwapiga na kuwatesa kwa madai
kuwa wananchi hao wanaipinga serikali.
Kubenea aliandika Makala hiyo baada
ya kusafiri kutoka Dar es Salaam Mpaka Zanzibar kufuatilia kile alichokitaja
kama mateso, unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wananchi
wasio na hatia visiwani humo.
Miongoni mwa vijana na wahanga wa
kubambikiwa kesi, kupigwa na kuteswa visiwani Pemba waliotajwa na Kubenea
katika makala yake ni ni Hijja Hassani aliyetangazwa kuwa ni Mwakilishi wa
Jimbo la Kiwani kabla ya Jecha Salim Jecha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi.

No comments:
Post a Comment