Nikiwa na Ray Kigosi wangu, huwa nahisi kama dunia yote ni yangu – Chuchu Hans - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 29 August 2016

Nikiwa na Ray Kigosi wangu, huwa nahisi kama dunia yote ni yangu – Chuchu Hans

       Ray akiwa na Chuchu Hans
Miss Tanga mwaka 2005, Chuchu Hans amesema kuwa ndani ya mahusiano ya kimapenzi na staa wa filamu, Ray Kigosi anajiona kama dunia yote ni yake.

Muigizaji huyo amesema anajisikia furaha sana jinsi anavyoishi kwa kusikilizana na mpenzi wake huyo.
“Nikiwa na Ray wangu, huwa nahisi kama dunia yote ni yangu, Ray ananidekeza sana,”Chuchu aliliambia gazeti la Mtamzania.“Ana mapenzi ya kweli, ananipenda mimi na watoto wangu wawili, amekuwa baba bora sana na hilo ndiyo linanifanya nijivunie na kuachana na maneno ya watu,”
Aliongeza, “Kufunga ndoa ni riziki na ninaamini haijafika siku yake, siku ikifika basi kila kitu kitakuwa wazi na hakuna atakayeweza kukwepa jambo hili, ila mapenzi na thamani tunayopeana ni ya mke na mume.”

Kwa sasa Chuchu na Ray Kigosi wamefunguka kampuni ya filamu iitwayo ‘Chura’.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here