
CHADEMA inapenda kutoa taarifa kwa
umma kuhusu andiko linalosambazwa mitandaoni likimnukuu Mwenyekiti wa Chama
Taifa, Freeman Mbowe kuwa ameahirisha Operesheni UKUTA na maandalizi ya
Septemba 1.
Tunaomba umma upate taarifa sahihi
kuwa Mwenyekiti Mbowe hajafanya mkutano na waandishi wa habari mahali popote
pale kuzungumzia kuahirisha Operesheni UKUTA inayoendela nchi nzima wala kuzuia
maandalizi ya Septemba 1.
Kupitia taarifa hii, chama
kinawataka viongozi, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA na
Watanzania wote wazalendo na wapenda haki, kupuuza andiko linalosambazwa
mitandaoni .
Msisitizo unaendelea kutolewa kuwa
Operesheni UKUTA ambayo imelenga kusimamia utawala unaoheshimu Katiba ya Nchi
na kulinda sheria na maandalizi yanaendelea nchi nzima.
Imetolewa na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na
Mawasiliano
CHADEMA

No comments:
Post a Comment