Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeeleza kuwa ifikapo Desemba 31 mwaka huu jumla ya watanzania milioni 23 watakuwa na namba za utambulisho wa vitambulisho vya Uraia.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Rose
Mdami amesema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo Rais, Dkt. John Pombe
Magufuli la kuitaka Mamlaka hiyo kuweka saini ya mwombaji na mtoaji wa
vitambulisho hivyo.
“Tumeanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais tangu mwezi Juni mwaka
huu, hii inamaanisha kwamba vitambulisho vyote tulivyochapisha kuanzia mwezi
Juni mpaka leo vina saini ya muombaji, saini ya mtoaji na tarehe ya kuzaliwa
muombaji” amefafanua
Mdami.
Ameeleza kuwa kazi ya ugawaji wa vitambulisho hivyo inasubiri
kuzinduliwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli atakayekabidhiwa
kitambulisho cha uraia namba moja na baadaye vitambulisho hivyo kugawiwa kwa
wananchi wengine.
Mdami amesema ifikapo Desemba 31 mwaka huu NIDA itakuwa imetoa
namba za utambulisho wa vitambulisho hivyo kwa watanzania milioni 23 kwa
kutumia taarifa za Tume ya Uchaguzi (NEC) zilizo katika vitambulisho vya
kupigia kura na kuziamishia katika kanzi data ya NIDA.
Amefafanua kuwa ili mwananchi aweze kupata kitambulisho
cha uraia atalazimika kufika katika ofisi za NIDA akiwa na vielelezo
vinavyoonyesha mwaka wake wa kuzaliwa pamoja uthibitisho wa uraia wake hii ni
kutokana na NEC kutokuwa na viambatanisho hivyo.
Amebainisha kuwa mwananchi mwenye namba ya utambulisho anaweza
kupata huduma zote zinazohitaji namba ya kitambulisho cha Uraia kutokana na
namba hiyo kutobadirika na kuendelea kutumika hata baada ya kitambulisho
kuchapishwa.
Amesema mpaka sasa watanzania milioni 2.7 wamekwisha patiwa
vitambulisho hivyo na milioni 6.5 wamesajiriwa kwa ajili ya kupata
vitambulisho hivyo.
Aidha, Vitambulisho hivyo vya zamani vitaendelea kutumika mpaka
utakapotangazwa utaratibu wa kuvibadirisha kwa ajili ya kupata vitambulisho
vipya.
Pia ametoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya baadhi ya watu
wanaodai kwamba wa kumekuwa na mlolongo mrefu wa kupata vitambulisho hivyo kwa
kueleza kuwa NIDA haina namna ya kufupisha mlolongo huo kwani kufanya hivyo ni
sawa na kuuza uraia wa Tanzania.
Amesisitiza kuwa ni lazima NIDA ijiridhishe juu ya uhalali
na sifa za muombaji ni kuwa ni Mtanzania kwa kuambatanisha vielelezo
vinavyohitajika.
No comments:
Post a Comment