
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Agosti, 2016 amemteua Bw.
Andrew Wilson Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA).
Kabla ya uteuzi huo Bw. Andrew
Wilson Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu
Tanzania (BOT).
Bw. Andrew Wilson Massawe anachukua
nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus Francis Kipilimba ambaye ameteuliwa
kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Uteuzi wa Bw. Andrew Wilson Massawe
unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi
wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
25 Agosti, 2016

No comments:
Post a Comment