Nchini Senegal, watu kadhaa wameandamana mjini Dakar kumuunga
mkono mwanamke mmoja raia wa nchi hiyo aliyekamatwa majuma machache yaliyopita
na kushtakiwa kwa makosa ya kumuua mke wa mwajiri wake huko Saudi Arabia.
Familia ya Mbayang Diop na wanaharakati wa haki za binaadam
wanahofu huenda akanyongwa kwa mujibu wa sheria za Saudi Arabia.
Ripoti ya kukamatwa kwa Mbayang Diop zilikuwa tayari kwenye
vyombo vya habari vya Senegal siku chache zilizopita.lakini sasa wanaharakati
wa masuala ya haki za binaadam wameanzisha kampeni kwenye mitandao ya kijamii
wakisihi kumuokoa Mbayang, kampeni ambayo imekuwepo kwa kipindi cha saa 24
zilizopita, kabla ya mkutano wa jumatatu uliofanyika kwenye msikiti mmoja wa
katikati mwa mji wa Dakar.
Wanasiasa wanawake, wakiwemo wale wanaotoka chama tawala na
upinzani, pia wafuasi wa asasi za kiraia na chama cha wafanyakazi wa majumbani
walikutana kwa ajili ya kesi ya binti wa miaka 22 , ambaye aliondoka Senegal
baada ya kuahidiwa kuwa atapata kazi nzuri inayolipa vizuri nchini Saudi
Arabia.Badala yake, kwa mujibu wa kaka yake, binti huyo alikuwa akinyanyaswa,
hivyo alimuua mke wa mwajiri wake baada ya kulumbana.
Mamlaka ya mambo ya nje ya Senegal imesema wanafuatilia kesi
hiyo kwa karibu na kutangaza kuwa Balozi wa Senegal nchini Saudi Arabia
atakutana na Mbayang siku ya jumatano gerezani anakoshikiliwa.
Wanaharakati wameomba huruma ya Serikali ya Senegal ili iweze
kuzungumza na mamlaka za Saudi Arabia ili binti huyo arudishwe nchini mwake na
kushtakiwa.
Hata hivyo mamlaka hazijasema hatua gani zitachukua.
Wanaharakati wa haki za binaadam, waliripoti visa vya
unyanyasaji wanavyofanyiwa wafanya kazi wa ndani kutoka nchini Senegal walioko
Saudi Arabia,Lebanon,Morocco na Algeria
No comments:
Post a Comment