
Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi, Prof Joyce Ndalichako amesema wizara hiyo imelazimika
kusitisha malipo ya fedha za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa elimu ya juu
kwa muda wa wiki mbili ili kupisha zoezi la uhakiki wa wanafunzi hewa
Amesema hadi sasa wanafunzi hewa
zaidi ya 2000 tayari wamebainika kwenye vyuo mbalimbali nchini na walikuwa
tayari kupokea fedha hizo jambo ambalo ni hasara kwa serikali.
Prof. Ndalichako amesema, tayari
amewaagiza wakuu wote wa vyuo kuwasilisha upya majina ya wanafunzi wanaostahili
kupatiwa fedha hizo bila udanganyifu.
Amefafanua kwamba, wamegundua
taarifa zilizopelekwa awali zilikuwa na udanganyifu hivyo serikali imelazimika
kusitisha zoezi la upelekaji fedha kwenye vyuo hivyo.
Kwa upande wa wanafunzi ambao vyuo
vyao vimefungiwa Prof. Ndalichako amesema tayari wametoa maelekezo ya
kuwasaidia kupata haki yao muhimu ya kusoma na kusisitiza hakuna mwanafunzi
hata mmoja ambaye atakosa msaada wa serikali

No comments:
Post a Comment