Bw Trump alikuwa akihutubu katika
mkutano wa siasa katika jimbo la North Carolina.
Bw Trump alikuwa amesema kwamba
iwapo Bi Clinton atashinda basi atateua majaji wa Mahakama ya Juu ambao
watafanikisha kuondolewa kwa haki ya raia kumiliki bunduki.
Alidokeza kwamba ni hatua ya raia
pekee, ambayo inaweza kuzuia hilo lisifanyike.
Maafisa wa kampeni wa Clinton
wameshutumu matamshi ya Trump na kusema ni hatari.
Lakini washauri wake wamesema
alikuwa tu anawahimiza watu wanaoamini katika haki ya raia kumiliki silaha
watumie kura zao kufanya uamuzi.

No comments:
Post a Comment