Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema (Chadema), amemuandikia waraka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Magufuli akimsihi kuruhusu kufanyika kwa mikutano ya kisiasa nchini
bila kujali mipaka ya majimbo.
Lema amepaza sauti yake kupitia
waraka wake kwa Rais Magufuli, uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, waraka
ambao alithibitisha kuwa ni wake.
Katika waraka huo, Lema ambaye pia
na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alimsihi Rais Magufuli kuviruhusu vyama vya
siasa kufanya mikutano hiyo kwani ni sehemu ya matakwa ya katiba.
Alitahadharisha kuwa endapo mambo
yaliyoruhusiwa kikatiba hayataruhusiwa, ipo siku amri za utekelezaji wa masuala
muhimu kikatiba hazitachukuliwa kwani hakutakuwa na sababu ya kuheshimu katiba
na utawala wa sheria.
“Kama hatuwezi kufanya
tunayoruhusiwa na Katiba, na anayetuzuia mamlaka yake yametokana na Katiba,
hakika mbegu inayopandwa ni hatari kwa ustawi wa Taifa, ipo siku amri ya
utekelezaji juu ya masuala muhimu haitachukuliwa kwa sababu umuhimu wa
kuheshimu katiba na utawala wa Sheria hautakuwepo,” aliandika.
Lema alimueleza Rais Magufuli kuwa
Siasa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na kwamba mfumo huo ndiyo chanzo cha
madaraka waliyonayo hapa nchini.
“Mheshimiwa Rais, siasa ni kazi na
ndiyo maana wewe ni rais kwa sababu ya siasa, na mimi ni mbunge kwa sababu ya
siasa, tena ni kazi muhimu sana tu kwani ndio mfumo pekee unaotafuta utawala wa
ngazi mbalimbali na wa juu kabisa katika nchi,”
Aidha, Lema alimsemea kwa Rais Magufuli
ambaye ni Mwenyekitiwa CCM, Msemaji wa chama hicho, Christopher Ole Sendeka kwa
kukiuka amri aliyoitoa Rais kwa kufanya mkutano Longido ambako sio jimbo lake.
“Mheshimiwa Rais, jambo hili
litaleta mpasuko katika taifa letu, ni kauli inayopaswa kurekebishwa haraka.
Hivi karibuni, msemaji wa CCM, Ole Sendeka alifanya mkutano Longido. Je, Ole
Sendeka ni Mbunge wa Longido? Au polisi wa Mkoa wa Arusha hawakusikia tamko
lake? "Alihoji.
Mbunge huyo alisisitiza kuwa
Chadema itafanya maandamano Septemba Mosi mwaka huu, huku akihoji madhara
yanayoweza kujitokeza siku hiyo, hivyo akamuomba Rais kutengua amri yake ya
kuzuia mikutano ya hadhara

No comments:
Post a Comment