WASANII mbalimbali wanaopenda amani
wameungana kwa pamoja kupinga maandamano ya UKUTA yanayotarajiwa kufanyika
Septemba Mosi, mwaka huu.
Akizungumza jana mbele ya Waandishi
wa Habari, Mwenyekiti wa Wasanii hao wapenda amani, Steve Nyerere alisema hamna
haja ya maandamano bali tunahaja ya kufanya kazi hususan kwa vijana.
"Vijana ndio muhimili mkubwa
kulinda amani ya nchi,tusiwaze maandamano bali tuwaze je Akinamama na Watoto
wanapata huduma hospitali"alihoji Steve Nyerere.
Kwa Upande wa Makamu Mwenyekiti wa
Wasanii hao, Asha Baraka alisema wameamua kupaza sauti zao kwa niaba ya Wasanii
wote wanaopenda amani.
Alisema Tanzania ni nchi ya Amani
sio nchi ya vita hivyo wanapofanya shughuli za UKUTA shughuli zote za kijamii
zitasimama.
Hatahivyo aliomba Septemba 1,
UKUTA wasimamishe maandamano hayo, pia watafute njia muafaka ya kuweza kuongea
Vyama kwa Vyama na wakapata muafaka ili nchi iweze kwenda mbele.


No comments:
Post a Comment