Birdman amedai kuwa Lil Wayne, ameihodhi album yake ya ‘Tha Carter V.’
Vyanzo vilivyo karibu na Birdman vimeiambia TMZ kuwa
vitisho vya Wayne kuacha muziki vimemshtua bosi huyo wa Cash Money, anayedai
kuwa madai kuwa ameishikilia album hiyo si ya kweli.
Vimesema ni Weezy ndiye mwenye kopi ya master ya album
hiyo, na hivyo Birdman anaona kama hahusiki nayo tena. Kwa upande wa Wayne,
imedaiwa kuwa yuko tayari kuwapa album hiyo lakini hadi alipwe chake.
Pia vyanzo hivyo vimedai kuwa Weezy hatoivujisha album
hiyo kwasababu hana mpango wa kuitoa bure. Awali, Wayne alidai dola milioni 8
kama advance na pia ikikamilika angepewa dola milioni 2. Kama atapewa kiasi
hicho cha fedha, basi album hiyo itatoka.
Wiki hii Lil Wayne alidai kuwa hawezi kuacha muziki
lakini hatofanya tena kazi na Birdman.
No comments:
Post a Comment