Mgombea urais wa chama cha Republican
nchini Marekani Donald Trump amesema baadaye wiki hii atatoa ripoti ya kina
kuhusu hali yake kimwili na kiafya.
Hata hivyo, amedokeza kwamba baada ya kupimwa, imebainika kwamba
uzani wake umezidi kiwango na anahitaji kupunguza.
Mgombea huyo alitoa muhtasari wa hali yake kiafya kwenye
karatasi ya ukurasa mmoja alipokuwa akishiriki katika kipindi cha televisheni cha
The Dr Oz Show.
Alimwambia mtangazaji kwamba uzani wake ni 236lb (kilo 107.048)
na kimo chake ni 6ft 3in, jambo linalomfanya kuwa na uzito kupita kiasi.
amesema anatumia dawa za kupunguza kiwango cha cholesterol
kwenye mwili wake, lakini yuko buheri wa afya.
Anadaiwa pia kuwa na viwango vya juu kuliko kawaida vya homoni
za testosterone.
Makala kamili ya mahojiano yake ya mtangazaji huyo itapeperushwa
hewani baadaye Alhamisi.
Maafisa wake wa kampeni wamesita kufichua yaliyomo kwenye
uchunguzi huo.
Bw Trump aliambia mkutano wa siasa mjini Canton, Ohio,
Jumatano usiku kwamba ana shaka kuhusu iwapo Bi Clinton, aliyezidiwa na kichomi
Jumapili na kulazimika kuahirisha mikutano ya kampeni, ana uwezo wa kuongoza
moja ya hafla zake.
Aliuliza umati: "Mnafikiri
Hillary angeweza kusimama hapa kwa saa moja na kufanya hivi? Sidhani, sidhani
anaweza."
Bw Trump baadaye alisema mgombea
huyo wa chama cha Democratic "analala kitandani, akiendelea kupata
nafuu".
No comments:
Post a Comment