Rapper Kalapina mmoja kati ya wadau ambao walimsaidia Chidi Benz
kumpeleka Sober House amefunguka kwa kusema kuwa kitendo cha Chidi Benz
kukatisha muda wa matibabu akiwa Sober House kumemkosesha vitu vingi pamoja na
kupelekwa Ulaya kwa ajili ya matibabu.
Akiongea
katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Jumanne hii, Kalapina amesema Chid
Benz alikuwa hajapata matibabu sahihi alipotoka ‘sober house’.
“Chid Benz hakumaliza muda wa
matibabu alivyotoka ‘sober house’ ndani ya siku 28, kwahiyo mi namuomba
afikirie faida alizozipata sober na faida anazozipata sasa hivi akiwa mtaani,
nafasi bado ipo kwake kwa sababu tumeplay part kubwa hadi Chid Benz akae sawa,
kwa hiyo anatakiwa atusikilize, nafasi ipo kubwa kwa Chid Benz kuweza
kujisahihisha”, alisema Kalapina.
Kalapina amesema Chidi Benz alipata
wafadhili wa kumpeleka nchi za nje kwa matibabu zaidi, lakini ikashindikana
kutokana na kitendo hicho.
“Kulikuwa kuna safari ya yeye na
Ray C kupelekwa Ulaya, wafadhili walikuwa wanataka kuwapeleka Ulaya kwa
matibabu zaidi, lakini ilitakiwa subira kidogo, ndani ya siku 28 yeye amechoka
kukaa sober anataka kukaa mtaani, sasa wafadhili wakishaona uko mtaani tena
ku’invest hela yao inakuwa ngumu wanaona bado hujapona”, alisema Kalapina
No comments:
Post a Comment