Daraja la vioo lililojengwa juu nchini Uchina ililosifiwa kwa kuvunja
rekodi lilipozinduliwa siku 13 tu zilizopita limefungwa.
maafisa wanasema serikali inapanga kufanya ukarabati wa
dharura wa eneo hilo na hivyo kufunga daraja hilo Ijumaa, ambapo tarehe ya
kufunguliwa tena itatangazwa.
Lakini Kituo cha televisheni cha Marekani CNN kimesema
kuwa msemaji amewaambia kuwa daaja hilo linaloelea juu “limekuwa likitembelewa
na wageni wengi kupita uwezo wake “.
Amesema kuwa hakuna ajali iliyowahi kutokea na daraja
halikuwa na ufa wala mpasuko wowote.
Daraja hilo lenye urefu wa mita 430, ambalo ujenzi wake
uligarimu $3.4 milioni, linaunganisha mabonde mawili ya milima ya Zhangjiajie,
katika jimbo la Hunan.
Daraja hilo Linaeloelea umbali wa mita 300 kutoka kwenye
bonde linasemekana kuwavutia sana waandaaji wa filamu.
Lilipofunguliwa lilisemekana kuwa daraja refu zaidi kwa
kimo na upana zaidi lililotengenezwa kwa vioo duniani.
No comments:
Post a Comment