
Katika harakati za kuhakikisha kuwa
Mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo na kwa Wakati, Mamlaka ya Mapato
Tanzania TRA imejiwekea mikakati mbalimbali ya kuongeza wigo wa vyanzo vya
Mapato pamoja na kukusanya Mapato kikamilifu.
Mikakati hiyo ni kama ifuatavyo;
Kulifanya eneo la Kariakoo kuwa
Mkoa Maalumu wa Kodi kutokana na eneo hilo kuwa kitovu cha biashara hapa nchini
na kuhakikisha kila mfanyabiashara anakuwa na Mashine ya Kielektroniki ya kodi
(EFDs) na kuitumia ipasavyo.
Katika kutekeleza hilo Mawakala wote
wa EFDs wamefungua ofisi ya pamoja katika jengo la Al-Falah Towers lililopo
mtaa wa Msimbazi Kariakoo ili kurahisisha upatikanaji wa mashine hizo na
kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika matumizi ya mashine
hizo.
Aidha Mkurugenzi wa Huduma na Elimu
kwa Mlipa kodi TRA Bw. Richard Kayombo ametoa wito kwa wananachi na
wafanyabiashara kujitokeza kuhakiki taarifa zao za usajili wa TIN kabla ya
Tarehe 15 Oktoba 2016 katika vituo vifuatavyo kwaajili ya zoezi hilo kwani muda
hautaongezwa baada ya tarehe hiyo maana baada ya tarehe hiyo zoezi hili
litahamia mikoa mingine;
Vituo hivyo vya uhakiki ni pamoja
na:
·
Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays
(Kariakoo-Gerezani)
·
Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo
Complex (Tegeta) na ofisi za TRA Kimara
·
Mkoa wa Kodi Temeke: Uwanja wa Taifa na Ofisi za TRA Mbagala-
Zakiemu
·
Wilaya ya Kigamboni – Ofisi za TRA Kigamboni
Pamoja na kuhakiki taarifa zao,
wafanyabiashara wote ambao hawana TIN nchini wanaombwa kufika katika ofisi ya
TRA iliyoko karibu nao ili kujisajili kuepuka kukumbwa na msako unaondelea hivi
sasa nchi nzima pamoja na uhamasishaji
Wakati huo huo Bw. Kayombo
amewahimiza wamiliki wa vituo vya mafuta kutekeleza agizo la Serikali la
kufunga mashine za EFDs kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba 2016 kwani kinyume
na hapo ukaguzi utaanza kufanyika kuanzia tarehe 1 oktoba na hatua za kisheria
zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kukiuka agizo hilo.
Katika kuhakikisha kwamba kodi ya
ongezeko la thamani VAT inakusanyawa kwa Wakati Mamlaka inawakumbusha
walipakodi wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani -VAT kuwasilisha
ritani ya kila mwezi kabla au tarehe 20 ya kila mwezi badala ya tarehe 27
iliyokuwepo kabla ya mwaka hu wa fedha.
Kwa upande wa walipa kodi zaa
makadirio na kodi za makampuni (Corpoaration Tax) wanakumbushwa kulipa kodi zao
mapema mwezi hu wa tisa badala ya kusubiri msongamano mwisho wa mwezi ambao
unaweza kuwasababishia usumbufu
Hivyo hivyo walipakodi wote
wanaodaiwa madeni ya kodi za nyuma au malimbikizo wanakumbushwa kutembelea
Mameneja wa mikoa, Wilaya na ofisi mbali mabli za TRA zinazowahudumia ili
kujadiliana namna ya kulipa madeni hayo.
Kutokana na mikakti mizuri
iliyowekwa na uiongozi wa TRA na serikali Mpaka sasa baadhi ya mikakati hiyo
imeanza kuonyesha mafanikio na mwelekeo mzuri wa makusanyo ambapo kwa kipindi
cha mwezi Agosti 2016 TRA imekusanya Trillioni 1.158 ikilinganishwa na lengo la
Trillion 1.152 ambayo ni asilimia 100.57 ambapo Mwezi Agosti Mwaka 2015
TRA ilikusanya Billion 923.
Wito wetu kwa wanahabari na
wananchi kwa ujumla ni kuendelea kutuunga mkono kwa kuhimiza kutoa risiti
pamoja na kudai risiti katika kila manunuzi pamoja na kutoa taarifa za dalili
za ukwepaji wa kodi wa aina yoyote mahali popote nchini
‘Pamoja Tunajenga
Taifa Letu’
Richard Kayombo
MKURUGENZI WA
HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI

No comments:
Post a Comment